• HABARI MPYA

  Thursday, April 29, 2021

  MANCHESTER CITY YAICHAPA PSG 2-1 PALE PALE PARIS

  TIMU ya Manchester City imetoka nyuma na kuwachapa wenyeji Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja Parc des Princes Jijini Paris nchini Ufaransa.
  PSG walitangulia kwa bao la Marquinhos dakika ya 15, kabla ya Kelvin De Bruyne kuisawazishia Man City dakika ya 64 na Riyad Mahrez kufunga la ushindi dakika ya 71.
  Man City watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo Uwanja wa Etihad. Ikumbukwe jana Real Madrid jana ililazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea Jijini Madrid nazo zitarudiana wiki ijayo London na washindi wa jumla wa mechi zote watakutana kwenye fainali Mei 29.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA PSG 2-1 PALE PALE PARIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top