TIMU ya Polisi Tanzania imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara licha ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Tanzania Prisons bao la Neva Kapoma dakika ya 86 jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Polisi Tanzania inanufaika na ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Mchujo wa mwisho wa kuwania kucheza Ligi Kuu Julai 12 Uwanjan wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mabao yake yakifungwa na Juhudi Philemon kwa penalti dakika ya sita, Tariq Seif dakika ya 46, Tatizo Shem dakika ya 54 na Emanuel Mpuka kwa penalti pia dakika ya 73.
Tanzania Prisons ilifikia kwenye mchujo huo baada ya kufungwa na Mbeya City kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchujo wa awali wa timu za igi Kuu tupu – wakati Polisi Tanzania iliitoa Mbeya Kwanza kwa jumla ya mabao 7-1 katika mchujo wa timu za Champonship tupu.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16, baada ya timu mbili za mwisho kuteremka, zinazofuatia katika nafasi ya 13 na 14 humenyana katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla anabaki kwenye ligi hiyo, wakati anayefungwa anakwenda kumenyana na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
Na kwenye Championship baada ya timu mbili za juu kupanda Ligi Kuu, zinazofuatia nafasi ya tatu na ya nne humenyana baina yao kwa michezo miwili ya nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla anakwenda kuwania kupanda Ligi Kuu dhidi ya timu iliyopoteza Mchujo wa Ligi Kuu – wakati inayofungwa inasalia Championship.
Kwa maana hiyo, timu zitakazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao ni; mabingwa watetezi, Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida Black Stars, TRA United, JKT Tanzania, Coastal Union, Pamba Jiji, Dodoma Jiji, Namungo FC, Mashujaa FC, Fountain Gate FC, Mbeya City, Geita Gold, Kagera Sugar, Polisi Tanzania baada ya kushuka kwa Mtibwa Sugar, KMC na Tanzania Prisons.



.png)
0 comments:
Post a Comment