• HABARI MPYA

  Wednesday, December 10, 2014

  PIGO LINGINE MAN UNITED, CHRIS SMALLING NJE WIKI MBILI

  BEKI wa Manchester United, Chris Smalling atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili baada ya kuumia nyonga usiku wa Jumatatu akiichezea timu yake dhidi ya Southampton katika Ligi Kuu ya England.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England ataikosa mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu dhidi ya mahasimu Liverpool Uwanja wa Old Trafford, na mechi itakayofuata dhidi ya Newcastle na labda pia atakosa mchezo wa Boxing Day nyumbani.
  Smalling anaumia tena baada tu ya kurejea uwanjani kufuatia kuwa nje kwa muea mrefu kwa maumivu ya misuli, jambo ambalo linaanza kuleta shaka labda ni sababu ya mazoezi magumu ya kocha wa United, Mholanzi Louis van Gaal. 
  Chris Smalling will be out for two weeks after an injury sustained at Southampton on Monday night 
  Chris Smalling atakuwa nje kwa wiki mbili baada ya juzi kuumia nyonga 


  Smalling anarudi tena nje baada ya kukosekana kwa muda mrefu sababu ya maumivu ya misuli

  Mashetani hao Wekundu, tayari kwa sasa wanawakosa nyota wao wapya, Angel di Maria, Daley Blind na Luke Shaw, ambao wote ni majeruhi, wakati Rafael na Phil Jones ndiyo kwanza wanarudi uwanjani baada ya kupona. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO LINGINE MAN UNITED, CHRIS SMALLING NJE WIKI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top