• HABARI MPYA

  Wednesday, December 24, 2014

  REFA WA MOMBASA AHITIMU KIWANGO CHA FIFA KENYA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  Mwamuzi msimamizi kutoka Mombasa, pwani ya Kenya, Joshua Achilla amejumuishwa katika orodha ya waamuzi wenye viwango vya FIFA nchini Kenya.
  Achilla anachukua nafasi yake Peter Kiereini kutoka milima ya Aberdares ambaye amesitaafu baada ya kutimu miaka 45, umri ambao FIFA imetenga kustaafu kwa waamuzi wenye viwango hivyo.
  “Joshua Achilla amejumlishwa kwenye orodha ya refa wa FIFA kutoka Kenya na anachukua nafasi yake Peter Kiereini aliyestaafu,” mwelekezi wa kamati la kiufundi la Shirikisho la Soka la Kenya, FKF, Elly Mukolwe aliambia BIN ZUBEIRY.
  Kenya ina wasimamzi kumi na wa saba wenye viwango vya FIFA; wanaume kumi na moja na wanadada sita.   

  ORODHA KAMILI
  WANAUME: Davies Omweno, Sylvester Kirwa, Andrew Juma, Anthony Ogwayo, Israel Mpaima.
  MAREFA WASAIDIZI: Joshua Achilla, Aden Marwa, Peter Sabatia, Gilbert Cheruiyot, Oliver Omondi, Tony Kidiya.
  WANADADA: Damaris Kimani, Tabitha Wambui, Agnetta Itubo.
  MAREFA WASAIDIZI: Mary Njoroge, Jane Cherono, Caroline Kiles.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA WA MOMBASA AHITIMU KIWANGO CHA FIFA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top