• HABARI MPYA

  Monday, December 22, 2014

  MBUYU TWITE ANAANZA MAZOEZI LEO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Mbuyu Twite anatarajiwa kuanza mazoezi leo, baada ya kuwa nje kwa wiki moja kufuatia kuumia kifundo cha mguu.
  Mbuyu Twite anayeweza kucheza kama beki wa pembeni na kati pia, aliumia Desemba 13 akiichezea klabu yake, Yanga SC dhidi ya mahasimu, Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
  Mbuyu Twite aligongwa na beki wa Simba SC, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Hassan Dilunga dakika ya 39, wakati huo tayari Yanga SC imefungwa 1-0 na mwisho wa mchezo ikalala 2-0. 
  Mbuyu Twite kushoto anaanza mazoezi leo

  Baada ya mapumziko na tiba ya wiki nzima, mchezaji huyo wa zamani wa APR ya Rwanda yuko tayari kurudi kazini, klabu yake ikikabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC Desemba 28, mwaka huu.
  Kurudi mapema kwa Twite ni faraja kwa Yanga SC, kwani tayari itamkosa Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBUYU TWITE ANAANZA MAZOEZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top