• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  RONALDO APANIA MAKUBWA ZAIDI 2015

  MWANASOKA bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba atajitahidi kuhakikisha mwaka 2015 unakuwa wa mwafanikio kwake kuliko 2014.
  Mchezaji huyo wa Ureno na Real Madrid anayewani kishinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya tatu na mara ya pili mfululizo, amesema hayo akiwa mapumziko Dubai. Ronaldo ameposti picha akiwa kwenye boti la kifahari nchini Dubai.
  Mshambuliaji huyo wa Ureno amekuwa na mwaka mzuri 2014, na amepania kuendeleza mafanikio hayo na mwakani pia.
  "Itakuwa ni ndoto iwapo 2015 utakuwa kama 2014 au mzuri zaidi," amesema Ronaldo katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la kila siku la michezo, As leo.
  Cristiano Ronaldo posted this image on Twitter from a yacht while enjoying a wintersun break in Dubai
  Cristiano Ronaldo ameposti picha hii katika akunti yake ya Twitter akiwa kwenye boti la kifahari huku akifurahia kijua chembamba nchini Dubai
  The forward kisses his third Golden Boot award for being the premier European scorer in 2014
  Ronaldo akibusu tuzo yake ya tatu ya Kiatu cha Dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora wa Ulaya mwaka 2014
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APANIA MAKUBWA ZAIDI 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top