// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAINGIA KAMBINI BAGAMOYO LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAINGIA KAMBINI BAGAMOYO LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 22, 2014

    YANGA SC WAINGIA KAMBINI BAGAMOYO LEO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC inakwenda kambini Bagamoyo mkoani Pwani leo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara raundi ya nane, dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC Desemba 28, mwaka huu.
    Yanga SC itakuwa katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo ikijifua mfululizo chini ya kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, ambaye anataka kurejesha mfumo wa kushambulia na soka ya kuburudisha ndani ya timu hiyo.
    Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, amerejeshwa Yanga SC wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Mbrazil, Marcio Maximo aliyeondolewa baada ya kutofautiana na uongozi.
    Nahodha wa Yanga SC kushoto, Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa na mshambuliaji mpya kutoka Liberia, Kpah Sherman

    Pluijm atafanya kazi na aliyekuwa Msaidizi wake awali akifanya kazi Yanga SC msimu uliopita, Charles Boniface Mkwasa baada ya Maximo kuondolewa pamoja na Msaidizi wake, Mbrazil mwenzake, Leonardo Leiva.
    Kuna uwezekano Yanga SC ikarudi mjini Jumatano kucheza mchezo wa kirafiki na Stand United ya Shinyanga, Uwanja wa Taifa.
    Pluijm amesema kwamba ameiona Yanga SC na akiwa ana muda wa wiki moja kabla ya kucheza na mabingwa watetezi, Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ana muda wa kutosha kurekebisha timu.
    “Nitatumia wiki hii tukiwa kambini kurekebisha timu na kurudisha mfumo wa kucheza kwa kushambulia na kuburudisha kwa soka nzuri, nataka nirejeshe heshima ya Yanga,”amesema.
    Amesema kwamba pamoja na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji kama Waganda, Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza, Mrundi Didier Kavumbangu na mzalendo Frank Domayo, Yanga bado ni timu nzuri.
    Lakini pia amesema Yanga SC imesajili wachezaji wengine wazuri ambao anaamini watawafanya mashabiki wa timu hiyo wawasahau wachezaji walioondoka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI BAGAMOYO LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top