• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  MWADUI YAITANDIKA TOTO 3-2, VILLA SQUAD WACHAPWA 1-0

  Na Mwandishi Wetu, MWADUI
  TIMU ya Mwadui ya Shinyanga imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya kuifunga Toto Africans mabao 3-2 mjini Mwadui, Shinyanga. 
  Matokeo hayo yanaifanya Mwadui inayofundishwa na kocha na beki wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo itimize pointi 25 baada ya kucheza mechi 12, wakati Toto inabaki na pointi zake 22 katika nafasi ya pili nyuma ya wapinzani wao hao.
  Mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Rhino imetoa sare ya 1-1 Polisi Mara, Polisi Dodoma imetoa sare ya na 1-1 JKT Oljoro, wakati Villa Squad imefungwa 1-0 na Kimondo.
  Kikosi cha Mwadui kimeanza vyema mzunguko wa pili Daraja la Kwanza

  Katika Ligi Daraja la Pili, Mbao imeilaza 2-1 JKT Rwamkoma, AFC imeifunga 1-0 Pamba, Mji Njombe imeshinda 2-0 dhidi ya Wenda, wakati mchezo kati ya Mkamba na Volcano umevunjika dakika ya sita kutokana na mvua na sasa utamaliziwa kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI YAITANDIKA TOTO 3-2, VILLA SQUAD WACHAPWA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top