• HABARI MPYA

  Thursday, December 25, 2014

  KIPA LA UGANDA CRANES LAONGEZA MKATABA THIKA UNITED

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  GOLIKIPA wa timu ya taifa la Uganda Hamuza Muwonge ameongeza mkataba wa miaka miwili kwenye timu yake ya Thika United inayoshiriki ligi kuu ya taifa la Kenya.
  Muwonge alijiunga na Thika United mapema mwakani kutokea klabu ya Vipers FC ya Uganda kwa mwaka mmoja na mkataba huo ulikuwa umeratibiwa kukamilika tarehe Desemba 31, lakini sasa atazidi kuwajibikia timu hiyo kwa misimu mingine miwili.
  Muwonge mwenye umri wa miaka 32 alichangia sana msimu uliyopita na kuiwezesha Thika United kumaliza katika nafasi nane bora kwa pointi 39 baada ya mechi 30.
  Kando na Muwonge, beki wa timu ya taifa la Kenya, Harambee Stars, na chipukizi Vincent Nyaberi Mogaka pia ameongeza mkataba wake.

  Vincent Nyaberi Mogaka pia ameongeza mkataba Thika United

  Klabu hiyo vile vile imepandandisha chipukizi Eugine Moses (kiungo) na beki Christopher Oruchum katika kikosi cha timu ya kwanza. Wawili hao wamekuwa katika kikosi chipukizi cha timu hiyo inayonolewa na kocha Moses Irungu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA LA UGANDA CRANES LAONGEZA MKATABA THIKA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top