• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  PLUIJM AMTABIRIA MEMA HAMISI KIIZA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza juzi alitua nchini kumalizana jumla na uongozi wa timu hiyo na kukutana na kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Pluijm ambaye amemwambia asijali atapata timu mpya haraka.
  Kiiza alikutana na Pluijm jana asubuhi ambapo katika maongezi yao yaliyochukua dakika tano Pluijm alimtakia kila la kheri huko aendako kwao Uganda huku akimtaka kutuliza akili kwa kuwa kwa uwezo alionao atapata timu.
  Pluijm akizungumza na Kiiza makao makuu ya Yanga SC
  Kiiza (kulia) alikuwa tegemeo la mabao Yanga SC

  "Huyu ni mchezaji mimi ni kocha kuondoka Yanga sio kwamba hatapata timu, Kiiza ni mchezaji mzuri lakini changamoto ndiyo zimemuondoa hapa naamini atapata timu mpya na atacheza vizuri,"alisema Pluijm.
  "Nilikutana naye hapa Yanga tena nikimkuta hapa lakini sasa tumepishana hayo ndiyo maisha yetu katika soka bado anaweza kucheza licha ya kwamba hapa Yanga hayupo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AMTABIRIA MEMA HAMISI KIIZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top