• HABARI MPYA

  Tuesday, December 30, 2014

  MAPINDUZI ‘YAISULUBU’ LIGI KUU BARA, MECHI ZA SIMBA, YANGA, AZAM ZAPIGWA ‘STOP’ VIKOSI VIENDE ZANZIBAR

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha mechi mbili za kila timu Azam FC, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015.
  Hatua hiyo ya TFF imefuatia timu hizo kugoma kucheza Kombe la Mapinduzi wakati huo huo zikiendelea na mechi za Ligi Kuu.
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, waandaaji wa mashindano hayo wakatumia ‘ubavu’ wao kuhakikisha michuano hiyo haizikosi timu za Bara na TFF ‘wakanywea’.
  Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, SImba SC ikifungwa na KCCA ya Uganda

  Sasa, mechi kati ya Azam FC na Mtibwa, Azam FC na Kagera Sugar, Mtibwa na Azam, Mtibwa na Prisons, Simba SC na Mgambo, Simba SC na Mbeya City, Yanga SC na Mbeya City na Yanga na Coastal Union zitawekwa viporo.
  TFF itazichomeka mechi hizo katikati ya wiki baada ya kumalizika kwa Kombe la Mapinduzi.
  Awali kulikuwa kuna tishio la kutofanyika kwa michuano ya Mapinduzi, kutokana na viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kupelekana Mahakamani, lakini kesi hiyo imeondolewa na mashindano yanaanza mapema Januari.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAPINDUZI ‘YAISULUBU’ LIGI KUU BARA, MECHI ZA SIMBA, YANGA, AZAM ZAPIGWA ‘STOP’ VIKOSI VIENDE ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top