• HABARI MPYA

  Sunday, December 28, 2014

  MBEYA CITY YAJINASUA MKIANI, POLISI MORO YAICHAPA MGAMBO 2-0

  MBEYA City imeibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
  Shukrani kwake, kiungo mshambuliaji Deus Kaseke aliyefunga bao hilo pekee na sasa MCC inatimiza pointi nane baada ya mechi nane, hivyo kujivuta hadi nafasi ya 11 kutoka mkiani. Ndanda inayobaki na pointi zake sita, sasa ndiyo inashika mkia.
  Katika mechi nyingine za Ligi hiyo leo, Yanga SC imetoka sare ya 2-2 na Azam FC. Mabao ya Yanga yamefungwa na Amisi Tambwe na Simon Msuva, wakati ya Azam FC yamefungwa na Didier Kavumbangu na John Bocco.
  Polisi Moro imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT, mabao yake yakifungwa na Nicholas Kabipe na Imani Mapunda. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAJINASUA MKIANI, POLISI MORO YAICHAPA MGAMBO 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top