• HABARI MPYA

  Wednesday, December 24, 2014

  ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA AFCON, SUNZU NDANI

  Na Mutheliso Phiri, LUSAKA
  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Zambia, Honor Janza amechanganya vijana na wazoefu katika kikosi cha awali cha wachezaji 27 kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 alichokitaja jana mjini Lusaka.
  Kikosi hicho kitakachopunguzwa hadi kubaki wachezaji 23 kufika Januari 10, kinatarajiwa kuanza kambi yake Desemba 26 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Zambia inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Bafana Bafana Januari 4 na Janza amechukua wachezaji 12 waliokuwa AFCON ya 2013 na 11 kutoka kikosi kilochotwaa Kombe hilo mwaka 2012.
  Stopila Sunzu ataiongoza Zambia katika AFCON mwakani

  Kikosi kamili cha Zambia ni makipa; Kennedy Mweene (Mamelodi Sundowns, RSA), Danny Munyau (Red Arrows), Toaster Nsabata (Nchanga Rangers) na Joshua Titima (Power Dynamos).
  Mabeki; Stoppila Sunzu (Sochaux, France), Bronson Chama (Red Arrows), Donashano Malama (Nkana), Aaron Katebe (FC Platinum, Zimbabwe), Christopher Munthali (Nkana), Emmanuel Mbola (Hapoel Ra'anana, Isreal), Davies Nkausu (Bloemfontein Celtic, RSA) na Rodrick Kabwe (Zanaco).
  Viungo ni; Nathan Sinkala (Grasshoppers, Switzerland), Chisamba Lungu (FC Ural, Russia), Mukuka Mulenga (Bloemfontein Celtic, RSA), Kondwani Mtonga (North East United, India), Spencer Sautu (Green Eagles), Rainford Kalaba (TP Mazembe, DRC) na Bruce Musakanya (Red Arrows), Lubambo Musonda (FC Ulisses, Armenia).
  Washambuliaji ni; Emmanuel Mayuka (Southampton, England), Given Singuluma (TP Mazembe, DRC), Ronald 'Sate Sate' Kampamba (Nkana), Evans Kangwa (Hapoel Ra'anana, Isreal), Patrick Ngoma (Red Arrows), Jackson Mwanza (Zesco United) na James Chamanga (Liaoning Whowin, China).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMBIA YATAJA KIKOSI CHA AFCON, SUNZU NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top