• HABARI MPYA

  Friday, December 26, 2014

  ARSENAL PUNGUFU YAIKALISHA QPR 2-1, GIROUD ALIMWA NYEKUNDU YA KUJITAKIA

  LICHA ya kuwa pungufu baada ya Olivier Giroud kutolewa kwa kadi nyekundu, Arsenal imemudu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya QPR katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates.
  Katika mchezo huo, Alexis Sanchez alikosa penalti mapema kipindi cha kwanza baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa Rob Green, baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi na Armand Traore.
  Sanchez alisahihisha makosa yake dakika ya 37 baada ya kuifungia The Gunners bao la kwanza akimalizia krosi ya Kieran Gibbs, kabla ya Giroud kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa kwa kumpiga kichwa Nedum Onuoha.
  Tomas Rosicky akaifungia bao la pili Arsenal dakika ya 65 akimalizia pasi nzuri ya Sanchez, kabla ya Charlie Austin kuifungia bao la kufutuia machozi QPR kwa penalti dakika ya 79. 
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny; Debuchy, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Flamini , Sanchez, Rosicky/Chambers dk83, Cazorla, Welbeck/Coquelin dk87 na Giroud.
  QPR; Green, Isla, Onuoha, Ferdinand, Caulker, Traore/Hoilett dk62, Mutch/Zamora dk72, Henry/Fer dk62, Kranjcar, Vargas na Austin.
  Rosicky (left) is congratulated by his Arsenal team-mates after doubling their advantage at the Emirates
  Rosicky (kushoto) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Arsenal leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL PUNGUFU YAIKALISHA QPR 2-1, GIROUD ALIMWA NYEKUNDU YA KUJITAKIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top