• HABARI MPYA

  Friday, December 26, 2014

  MECHI YA JKT RUVU, SHOOTING KUCHEZWA USIKU

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting itachezwa kesho (Desemba 27 mwaka huu) usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
  Timu hizo zitapambana kuanzia saa 1:00 Usiku katika mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.
  Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa jukwaa la kawaida na sh. 5,000 kwa upande wa jukwaa la VIP.
  Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ambazo ni za elektoniki tayari zimeanza kuuzwa kupitia maduka ya Fahari Huduma, M-PESA kwa kupiga *150*03*02# ambayo utapata namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kufanya malipo kupitia hiyo hiyo M-PESA na baadaye kuchapa tiketi yako katika mashine maalumu zilizopo kwenye ATM za CRDB.
  Kikosi cha JKT Ruvu

  Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kupitia CRDB Simbanking.
  Mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Abdallah Uhako (Arusha), Godwill Kihwili (Arusha) na Hashim Abdallah (Dar es Salaam).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA JKT RUVU, SHOOTING KUCHEZWA USIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top