• HABARI MPYA

  Tuesday, December 23, 2014

  MWADUI NA STAND UNITED ZAPIMANA KESHO KAMBARAGE

  Na Philipo Chimi, SHINYANGA
  ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, timu za Stand United na Mwadui FC kesho zitacheza mchezo wa kirafiki Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Akizungumzia mchezo huo na maandalizi kwa ujumla, kocha mpya wa Stand Utd ya Ligi Kuu, Mathia Lule amesema kwamba timu yake ipo vizuri na wamejiandaa vyema kutoa burudani kwa wapenzi wa soka mkoani humo.
  Amesema kuwa japo ni muda mfupi baada ya kutua katika timu hiyo juzi akitokea Express ya nchini kwao, Uganda tayari amekwishaanza kukiweka sawa kikosi hicho na kwamba kesho atawaonyesha wana Shinyanga uwezo wake.
  Kikois cha Mwadui FC ambacho kitamenyana na Stand United

  Kwa upande wake, kocha wa Mwadui FC ya Daraja la Kwanza kutoka wilayani Kishapu mkoani humo, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema anaamini kikosi chake kipo sawa kutokana na usajili walioufanya katika dirisha dogo na mechi ya kesho watafanya vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI NA STAND UNITED ZAPIMANA KESHO KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top