• HABARI MPYA

  Monday, December 22, 2014

  YANGA SC WAKIVUKA SALAMA BOTSWANA WATAKUTANA NA WAZIMBABWE

  YANGA SC ya Tanzania, itamenyana Sofapaka ya Kenya au Platinum ya Zimbabwe ikifanikiwa kuwatoa vibonde BDF IX ya Botswana katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani. 
  Kwa mujibu wa ratiba ya Raundi ya Awali iliyopangwa leo mjini Cairo, mechi za kwanza zitachezwa kati ya Februari 13 na 15 wakati marudiano yatakuwa Februari 27 na Machi 1 na Yanga SC itaanzia nyumbani dhidi ya timu ya jeshi la Botswana.
  Ikifanikiwa kuvuka mtihani huo, Yanga itamenyana na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya Platinum ya Zimbabwe katika kuwania kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAKIVUKA SALAMA BOTSWANA WATAKUTANA NA WAZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top