• HABARI MPYA

    Friday, December 26, 2014

    ATUPELE WA YANGA AIANGAMIZA SIMBA SC TAIFA

    Atupele aliibukia Yanga B
    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imeonyesha bado haiko tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni leo kuchapwa bao 1-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Huo ni mchezo wa kwanza kwa Simba SC kupoteza katika msimu huu baada ya mechi nane, lakini imeshinda mechi moja na kutoa sare sita awali, hivyo inabaki na pointi zake tisa. 
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, hadi mapumziko Kagera Sugar walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga B, Atupele Green.
    Atupele alifunga bao hilo kwa shuti akimalizia mpira wa kurushwa na Benjamin Asukile, ambao kabla ya kuingia nyavuni ulimbabatiza beki wa Simba SC, Hassan Isihaka.
    Kipindi cha pili, Kocha wa Simba SC Mzambia Patrick Phiri alianza na mabadiliko akimpumzisha kiungo Ramashani Singano ‘Messi’ na kumuingiza mshambuliaji Elias Maguri.
    Baada ya kuona mambo hayaendi kama alivyotarajia, kocha Phiri akafanya mabadiliko mengine dakika tano baadaye, akiwapumzisha Awadh Juma na Dan Sserunkuma na kuwaingiza Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Said Ndemla.
    Kocha wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja alifanya mabadiliko ya kwanza dakika ya 70, akimpumzisha Benjamin Asukile aliyeumia na nafasi yake kumuingiza Victor Hussein.
    Ndemla alikaribia kuifungia Simba SC bao la kusawazisha dakika ya 77 baada ya kupata pasi nzuri ya Hassan Ramadhan Kessy, lakini akapiga mpira juu ya lango.
    Kagera Sugar ilipata pigo dakika ya 88 baada ya mchezaji wake Babu Ali Seif kuumia na kupoteza fahamu kiasi cha kusababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu, kabla ya kutolewa na nafasi yake kuingia Simon Lucas.
    Mayanja akafanya mabadiliko mengine dakika ya 89, akumuingiza Juma Mpola kuchukua nafasi ya Daud Jumanne.   
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Ramadhan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Ramadhani SIngano ‘Messi’/Elias Maguri dk46, Awadh Juma/Shaaban Kisiga ‘Malone’ dk50, Dan Sserunkuma/Said Ndemla dk50, Simon Sserunkuma na Emmanuwl Okwi.
    Kagera Sugar; Agaton Anthony, Salum Kanoni, Abubakar Mtiro, Erci Kyaruzi, George Kavilla, Malegesi Mwangwa, Paul Ngway, Babu Ali Seif, Atupele Green, Daud Jumanne na Benjamin Asukile.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ATUPELE WA YANGA AIANGAMIZA SIMBA SC TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top