• HABARI MPYA

  Monday, December 22, 2014

  AZAM FC IKIWATOA MERREIKH ITAKUTANA NA WAANGOLA

  MABINGWA wa Tanzania, Azam  FC watamenyana Lydia Ludic B.A. ya Burundi au Kabuscorp do Palanca ya Angola wakifanikiwa kuitoa El Merreikh ya Sudan katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani. 
  Kwa mujibu wa ratiba ya Raundi ya Awali iliyopangwa leo mjini Cairo, mechi za kwanza zitachezwa kati ya Februari 13 na 15 wakati marudiano yatakuwa Februari 27 na Machi 1 na Azam FC wataanzia nyumbani.
  Wakifanikiwa kuwatoa Wasudan hao, Azam FC watamenyana na mshindi kati ya Lydia Ludic B.A. na Kabuscorp do Palanca.
  Ikumbukwe Azam FC ilitolewa na Merreikh katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Agosti mwaka huu mjini Kigali, Rwanda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. 
  Baadaye Azam FC ikamchukua beki wa Merreikh, Serge Wawa Pascal raia wa Ivory Coast (pichani juu) na ikamkosa kidogo mshambuliaji Mohamed Traore kutoka Mali- hivyo mechi baina ya timu inatarajiwa kuwa mpinzani mkali. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC IKIWATOA MERREIKH ITAKUTANA NA WAANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top