• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  EL SHAARAWYB APIGA MBILI MILAN IKIIFUMUA 4-2 REAL MADRID DUBAI

  TIMU ya Real Madrid imefungwa mabao 4-2 na AC Milan katika mchezo wa kirafiki Dubai uliochezwa katika mapumziko ya majira ya baridi.
  Jeremy Menez aliifungia Milan bao la kwanza kabla dakika ya 24 ya Stephan El Shaarawy kuongeza la pili dakika ya 31.
  Cristiano Ronaldo akaifungia la kwanza timu ya Carlo Ancelotti dakika 10 kabla ya mapumziko kabla ya El Shaarawy kufunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 49 na la tatu kwa Milan kipindi cha pili.
  Giampaolo Pazzini aliyetokea benchi aligongeana vizuri na M'Baye Niang kuifungia Milan bao la nne dakika ya 72, kabla ya Karim Benzema kuifungia Real kwa penalti dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho. 
  AC Milan captain Riccardo Montolivo holds aloft the Dubai Football Challenge trophy after beating Real Madrid 4-2
  Nahodha wa AC Milan, Riccardo Montolivo akiwa ameiinua Kombe la Dubai Football Challenge baada ya kuifunga Real Madrid 4-2
  Stephan El Shaarawy scored twice for AC Milan as they beat La Liga leaders Real Madrid 4-2 in a friendly on Tuesday evening
  Stephan El Shaarawy ameifungia AC Milan mabao mawili dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Real Madrid 4-2 katika mchezo wa kirafiki jana

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2891533/Real-Madrid-2-4-AC-Milan-Stephane-El-Shaarawy-scores-twice-Cristiano-Ronaldo-lose-time-September.html#ixzz3NSccfTWr 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EL SHAARAWYB APIGA MBILI MILAN IKIIFUMUA 4-2 REAL MADRID DUBAI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top