• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  HANS POPPE: MALINZI AMEPANIA KUTUMALIZA SIMBA SC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi hataki kuona mtu yeyote wa klabu hiyo katika shirikisho hilo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Hans Poppe amesema katika kuhakikisha anafanikisha mpango huo, Malinzi ameanza na zoezi la kwaondoa kwenye Kamati ndogo ndogo za TFF watu wote wa Simba SC.
  “Tayari hapa ninazo taarifa kwamba amebadilisha Kamati zote ndogo ndogo na amewaondoa watu wa Simba nikiwemo mimi,”amesema Hans Poppe ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.
  Zacharia Hans Poppe kushoto amesema kwamba Malinzi hawataki Simba SC TFF

  Kamati hiyo awali ilikuwa inaundwa na Mwenyekiti Wakili Richard Sinamtwa, Makamu wake, Wakili Moses Kaluwa na Wajumbe Hans Poppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Wakili Imani Madega.
  Lakini kwa mujibu wa Habari kutoka kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF mwishoni mwa wiki, Kamati hiyo sasa itaendelea kuwa chini ya Mwenyekiti Sinamtwa, lakini Makamu wake atakuwa Wakili Iddi Mandi na Wajumbe Nassor Idriss ‘Father’, Pascal Kihanga na Benister Lugora.
  Kamati hiyo pia itabadilika kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji hadi kuwa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji. Juhudi za kumpata Malinzi kuzungumzia hilo hazikufanikiwa mapema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE: MALINZI AMEPANIA KUTUMALIZA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top