// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIVERPOOL CHUPUCHUPU KUFA KWA ARSENAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIVERPOOL CHUPUCHUPU KUFA KWA ARSENAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 21, 2014

    LIVERPOOL CHUPUCHUPU KUFA KWA ARSENAL

    BAO la dakika ya 90+7 la beki Martin Skrtel limeinusuru Liverpool kulala nyumbani Uwanja wa Anfield baada ya kupata sare ya 2-2 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Beki huyo wa kati, Skrtel alifunga bao hilo muda mfupi tu baada ya Liverpool kumpoteza Fabio Borini aliyetolewa kwa kadi ya pili ya njano, akimalizia pasi ya Adam Lallana.  
    Philippe Coutinho alianza kuifungia Liverpool dakika ya 45 kwa pasi ya Jordan Henderson, kabla ya Mathieu Debuchy kuisawazishia Arsenal sekunde chache tu baadaye kabla ya kipyenga cha mapumziko akimalizia pasi ya Mathieu Flamini.
    Flamini alinusurika kutolewa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Adam Lallana, kabla ya Olivier Giroud kuifungia The Gunners bao la pili dakika ya 65.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Jones, Toure, Skrtel, Sakho, Lucas, Henderson, Markovic, Coutinho, Gerrard, Lallana na Sterling.
    Arsenal; Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Chambers, Gibbs, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Alexis, Giroud na Welbeck.
    Liverpool defender Martin Skrtel jumps above the Arsenal backline to power home a late leveller with his head and claim a point
    Martin Skrtel akiruka juu ya mabeki wa Arsenal kuifungia Liverpool bao la kusawazisha katika sare ya 2-2
    Liverpool centre backSkrtel celebrates after scoring a dramatic late equaliser against Arsenal in injury time
    Beki wa kati wa Liverpool, Martin Skrtel akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Arsenal dakika za majeruhi

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2882684/Liverpool-2-2-Arsenal-Martin-Skrtel-heads-injury-time-equaliser-claim-dramatic-late-point-Brendan-Rodgers-side.html#ixzz3MYc2RnoR 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL CHUPUCHUPU KUFA KWA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top