• HABARI MPYA

    Wednesday, December 24, 2014

    JAVU APIGA HAT TRICK, TAMBWE NA SHERMAN WAFUNGA MABAO YA KUSISIMUA ‘MECHI MAZOEZI’ YANGA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Hussein Javu (pichani kulia) amefunga mabao matatu peke yake katika sare ya 3-3 kwenye ‘mechi mazoezi’ Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam.
    Wachezaji wapya wa kigeni wa Yanga SC, Mrundi Amisi Joselyn Tambwe na Mliberia Kpah Sean Sherman nao wamefunga mabao mazuri katika mazoezi hayo.
    Yanga SC imeweka kambi hoteli ya Kiromo, Bagamoyo, mkoani Pwani lakini inafanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Na leo jioni, kocha Mholanzi Hans van der Pluijm alipanga vikosi viwili vimenyane kuelekea mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC Desemba 28, mwaka huu.
    Katika ‘mechi mazoezi’ hiyo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3.   
    Kikosi cha kwanza kikundwa na Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Mbuyu Twite, Kevin Yondani, Said Juma ‘Kizota’, Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Amissi Tambwe, Kpah Sherman na Dany Mrwanda.
    Kpah Sherman katikati ya Salum Telela na Nizar Khalfan kulia


    Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga akizungumza na kocha Pluijm baada ya mazoezi

    Mabao yao yalifungwa na Tambwe dakika ya 24 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ngassa, ambaye naye dakika ya 26 akawachambua mabeki baada ya kupokea pasi ya Msuva na kufunga  bao la pili, kabla ya Sherman kufunga la tatu dakika ya 30 kwa pasi ya Msuva.
    Kikosi cha pili kiliundwa na Ally Mustafa ‘Barthez’, Salum Telela, Oscar Joshua, Patrick Ngonyani, Rajab Zahir, Hassan Dilunga, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Hussein Javu, Jerry Tegete na Andrey Coutinho.
    Mabao yao yalifungwa yote na Javu aliyepiga dakika za tano pasi ya Oscar, dakika ya 40 pasi ya Niyonzima, dakika ya 59 pasi ya Tegete.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JAVU APIGA HAT TRICK, TAMBWE NA SHERMAN WAFUNGA MABAO YA KUSISIMUA ‘MECHI MAZOEZI’ YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top