• HABARI MPYA

  Thursday, December 25, 2014

  DAKTARI YANGA ASEMA; “HALI YA TAMBWE SHWARI”

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  HOFU ya Yanga kumkosa mshambuliaji wao mpya Amissi Tambwe katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Mabingwa watetezi Azam FC imepungua baada ya hali yake kuimarika huku matibabu zaidi yakifanyika kuhakikisha anakuwa sawa.
  Daktari wa Yanga SC, Juma Sufiani ameiambia BIN ZUBEIRY  kuwa hali ya  Tambwe ambaye alipata maumivu jana jioni katika mazoezi ya timu hiyo imeimarika ambapo sasa analazimika kupata matibabu ya haraka ambayo yatamfanya kuwa tayari kwa mechi hiyo.
  Sufiani alisema Tambwe ambaye aliumizwa katika paja lakela kushoto na beki wa timu Rajab Zahir ameonyesha kutohofia majeraha hayo ambapo amekiri kwamba kuna unafuu mkubwa wa maumivu hayo.
  Dk Sufiani akimtibu Tambwe jana Uwanja wa Boko Veterani

  "Tunajua kwamba hata iweje atapona lakini tunachotaka hapa kuona anapona kwa haraka zaidi, hatutaki kulazimisha lakini kutokana na hali aliyoamka nayo leo asubuhi mpaka mchana huu tunaamini kwamba atakuwa tayari mpaka Jumapili,"alisema Sufiani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAKTARI YANGA ASEMA; “HALI YA TAMBWE SHWARI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top