TIMU ya Algeria imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Fainali za Kombe la Dunia kufuatia sare ya kufungana mabao 3-3 na Austria katika mchezo wa mwisho wa Kundi J Alfajiri ya leo Uwanja wa Arrowhead Jijini Kansas City, Mossouri, Marekani.
Mabao ya Algeria yamefungwa na beki wa Hellas Verona ya Italia, Rafik Belghali mzaliwa wa Ubelgiji dakika ya 45 na winga wa Al-Ahli ya Saudi Arabia, Riyad Karim Mahrez mzaliwa wa Ufaransa, aliyefunga mawili dakika ya 60 na 90’+3.
Kwa upande wao Austria mabao yao yamefungwa na mshambuliaji Marko Arnautović wa Red Star Belgrade ya Serbia anakotokea baba yake dakika ya 28, kiungo Marcel Sabitzer wa Borussia Dortmund ya Ujerumani dakika ya 55 na mshambuliaji Sasa Kalajdzic mwenye asili ya Serbia anayecheza kwa mkopo LASK ya Austria kutoka Wolverhampton Wanderers ya England dakika ya 90’+6.
Mchezo mwingine wa Kundi J, Argentina imeichapa Jordan mabao 3-1 Uwanja wa AT&T, Arlington, Texas nchini Marekani.
Mabao ya Argentina yamefungwa na kiungo washambuliaji, Giovani Lo Celso wa Real Betis ya Hispania dakika ya 19, Lautaro Javier Martínez wa Inter Milan ya Italia dakika ya 31 kwa penalti na Lionel Andrés Messi wa Inter Miami ya Marekani dakika ya 80, wakati bao pekee la Jordan limefungwa na winga wa Rennes ya Ufaransa, Musa Mohammad Sulaiman Al-Taamari dakika ya 55.



.png)
0 comments:
Post a Comment