• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  KIPA WA TUSKER AHAMIA GOR MAHIA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  MABINGWA wa ligi kuu ya Kenya, Gor Mahia, wamemsajili mlindamlango wa Tusker FC Boniface Oluoch (pichani chini).
  Oluoch ambaye ameichezea timu ya taifa la Kenya, Harambee Stars mara sita ametia wino kwenye mkataba wa miaka miwili baada ya wake kukamilika Tusker.
  “Mkataba wangu ulikamilika na Tusker msimu uliyopita na Gor Mahia wakabisha ndiposa tukazungumza na tukaelewana na sasa nitakuwa najiunga nao msimu ujao,” Oluoch aliliambia BIN ZUBEIRY kwa njia ya simu.

  Kipa huyo, mshindi wa tuzo bora ya magolikipa miaka miwili kwa mfululizo, 2011 na 2012, hajakuwa na msimu mzuri wa 2014 na wanavileo hao. Kati ya mechi 30, alicheza mechi moja tu na ya mwisho ya ligi dhidi ya Sofapaka na sasa amehamisha makao yake ya miaka mitano kwenye klabu hiyo iliyoko Ruaraka kilomita kadhaa kutoka mjini Nairobi hadi katikati mwa mji kwa Gor Mahia.
  Kando na Oluoch, Gor maarufu kama K’Ogalo imo mbioni pia kuwanasa Khalid Aucho, Dirkir Glay (Thika United) na Robert Ssentongo kutoka URA FC ya Uganda miongoni mwa wachezaji wengine huku wakikamilisha orodha yao itakayoakilisha taifa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika watakapomenyana na CNAPs ya Madagascar kwenye awamu ya kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA WA TUSKER AHAMIA GOR MAHIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top