• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  MUINGEREZA KOCHA MPYA THIKA UNITED

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  KOCHA Muingereza Tim Bryett ndiye mkufunzi mpya wa klabu ya ligi kuu ya taifa la Kenya, Thika United.
  Bryett anachukua nafasi yake John Kamau aliyepata posho Posta Rangers mapema mwezi huu wa Desemba.
  “Thika United FC imepata huduma za Muingereza Tim Bryett. Kocha Bryett anachukua nafasi iliyoachwa wazi na John Kamau kama kocha mkuu,” tovuti ya klabu hiyo ilieleza.
  Bryett amewahi kuifunza klabu nyingine ya ligi kuu Kenya, Nairobi City Stars,  kabla ya kubwaga manyanga mwezi Agosti kwa kile alichoeleza kama vitina kutoka wenzake kwenye benchi la kiufundi.

  Muingereza Tim Bryett ndiye kocha mpya wa Thika United

  Kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Wycombe Wanderers na Academia ya Reading FC kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 na 20 anatarajia kuanza kazi rasmi Januari 5 timu ikirejea mazoezinii kujianda kwa msimu wa 2015.
  Ana leseni za UEFA ‘B’, CAF ‘A’ na shahada katika viwanda vya Spoti na mafunzo ya soka. 
  Thika United inayodhaminiwa na Brookside ilimaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu Kenya kwa pointi 39 baada ya mechi 30. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUINGEREZA KOCHA MPYA THIKA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top