• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  BEKI NEWCASTLE AJIGONGA KWENYE NGUZO NA KUCHANIKA JICHO

  BEKI wa Newcastle, Steven Taylor amechanika karibu na jicho baada ya kujigonga kwenye nguzo ya lango kipindi cha pili jioni ya leo katika mchezo dhidi ya mahasimu, Sunderland Uwanja wa St James' Park.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alifanikiwa kumzuia Steven Fletcher kuwafungia Sunderland wakati huo timu hizo zikiwa hazijafungana, lakini akachanika eneo la jichoni.
  Taylor mara moja alipata huduma ya kwanza kutoka kwa timu ya madaktari wa Newcastle kabla ya kutolewa nje na kutibiwa kwa dakika saba kisha kurejea uwanjani na kushangiliwa kishujaa na mashabiki wa timu yake. Newcastle ililala 1-0, bao pekee la Adan Johnson. 
  Newcastle defender Steven Taylor had a nasty collision with the post during the second-half
  Beki wa Newcastle, Steven Taylor akijigonga kwenye nguzo wakati wa kuokoa bao
  Taylor receives attention from the Newcastle medical team after the collision cut his eye and cheek
  Taylor akipatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa Newcastle baada ya kuchanika eneo la jichoni
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI NEWCASTLE AJIGONGA KWENYE NGUZO NA KUCHANIKA JICHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top