• HABARI MPYA

  Tuesday, December 23, 2014

  DK TIBOHORA: NATAKA YANGA SC IJIENDESHE KIUCHUMI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KATIBU Mkuu mpya wa Yanga SC, Jonas Tibohora leo amejitambulisha rasmi kwa uma kuanza kazi katika klabu hiyo lakini hapohapo akatangaza mikakati yake akitaka kwanza Yanga kujiendesha kiuchumi.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam Tibohora amesema kwamba Yanga haina sababu ya kuwa nyuma kimaendeleo kutokana na kila kitu kinachohitajika kuwepo katika klabu hiyo ambapo sasa anataka kufufua mipango thabiti ya kiunchumi iliyolala kwa muda mrefu.
  Katibu wa Yanga SC, Jonas Tibohora kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jangwani. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Jerry Muro.

  Tibohora ambaye kitaaluma ni daktari alisema katika mpango wake huo anataka kwanza kuhakikisha Yanga inakuwa na timu imara ambayo itasimama kupitia soka la vijana ambapo timu hiyo itakuwa na vikosi vya Yanga A,B na C.
  "Miaka minne iliyopita nilikuja hapa nikakutana na katibu aliyekuwepo wakati huo nikamwambia kwamba kuna kijana mdogo anaitwa Msuva (Simon) ninaye katika timu yangu ya vijana, nia yangu wamchukue lakini akapuuza na kuniambia ananitafuta,"alisema Tibohora.
  "Baadaye wakati michuano ya Uhai inataka kuanza katibu huyo akanifuata akitaka sasa nimpeleke huyo kijana bahati mbaya alikuwa ameshachelewa Moro United walikuwa tayari wameshamchukua baadaye mchezaji huyo huyo Yanga walikuja kumnunua kwa mamilioni.
  Aidha Tibohora alisema kutokana na safu yake mpya ya uongozi anataka kuhakikisha katika kipindi watakachokuwa madarakani Yanga inasimama kiuchumi ambapo hilo litatokana na usimamizi thabiti wa nembo ya klabu yao ambayo sasa inatumiwa na watu wasioinufaisha klabu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DK TIBOHORA: NATAKA YANGA SC IJIENDESHE KIUCHUMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top