• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  CAMEROON YAZIBA KIRAKA KIKOSI CHA AFCON

   BEKI Aurelien Chedjou (pichani kushoto) ameitwa kwenye kikosi cha Cameroon jana baada ya kutoitwa kwa miezi sita ili akazibe pengo la Brice Nlate kuelekea Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
  Chedjou hajaichezea nchi yake tangu Kombe la Dunia mwaka huu, lakini kuumia goti kwa Nlate katika ajali ya gari kiasi cha kutoweza kushiriki michuano hiyo ya timu 16 Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 kunamrudisha kikosini.
  Chedjou mwenye umri wa miaka 29, anayechezea Galatasaray ya Uturuki, ni miongoni mwa wachezaji wakongwe ambao muda wao kuichezea timu ya taifa ulionekana kupita, baada ya Cameroon kufungwa mechi zote tatu za kundi lake kwenye Kombe la Dunia Brazil.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAZIBA KIRAKA KIKOSI CHA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top