• HABARI MPYA

  Saturday, December 27, 2014

  DEMBA BA ATEMWA SENEGAL KIKOSI CHA AFCON

  Na Mwandishi Wetu, DAKAR
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea na Newcastle, Demba Ba ametemwa katika kikosi cha wachezaji 28 cha Senegal kilichotajwa na kocha Alain Giresse jana kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika.
  Mzaliwa huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa katika kiwango cha juu katika klabu yake, Besiktas katika michuano yote, Ligi ya Uturuki na Europa League na alicheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2012 mechi zote tatu za Raundi ya kwanza.
  Mchezaji mwenzake wa zamani Ba, mshambuliaji wa Newcastle, Papiss Cisse, ndiye nyota wa kikosi hicho kwa sasa kwa mabao yake 16 aliyofunga katika mechi 31.
  Demba Ba ametemwa kwenye kikosi cha Senegal

  Giresse, aliyeanza kazi Simba wa Teranga Januari mwaka 2013, amemuita mchezaji mmoja tu anayecheza nyumbani, kipa wa Diambars, Ousmane Mane.
  Senegal imepangwa Kundi C pamoja na Afrika Kusini, Ghana na Algeria kwenye michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Januari 17 hadi Februari 8 nchini Equatorial Guinea.
  Senegal iliingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002, mwaka ambao pia walifika Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Mali na kufungwa na Cameroon kwa penalti.
  Kikosi kamili cha awali cha Senegal kinaundwa na makipa; Bouna Coundoul (Ethnikos Achnas FC/Cyprus), Lys Gomis (Trappani/Italia), Pape Demba Camara (Sochaux/Ufaransa), Ousmane Mane (Diambars).
  Mabeki; Zargo Toure (Le Havre/Ufaransa), Lamine Gassama (Lorient/Ufaransa), Lamine Sane (Bordeaux/Ufaransa), Kara Mbodj (Genk/Ubelgiji), Pape Ndiaye Souare (Lille/Ufaransa), Papy Djilobodji (Nantes/Ufaransa), Boukary Drame (Atalanta/Italia), Ibrahima Mbaye (Inter Milan/Italia), Cheikh Mbengue (Rennes/Ufaransa).
  Viungo; Cheikhou Kouyate (West Ham Utd/England), Pape Kouli Diop (Levante/Hispania), Idrissa Gana Gueye (Lille/Ufaransa), Stephane Badji (Brann/Norway), Salif Sane (Hanover/Ujerumani), Pape Alioune Ndiaye (Bodo Glimt/Norway), Alfred Ndiaye (Real Betis/Hispania).
  Washambuliaji; Moussa Konate (SC Sion/SUI), Diafra Sakho (West Ham Utd/England), Mame Birame Diouf (Stoke City/England), Sadio Mane (Southampton/England), Moussa Sow (Fenerbahce/Uturuki), Papiss Demba Cisse (Newcastle Utd/England), Henri Saivet (Bordeaux/Ufaransa), Dame Ndoye (Lokomotiv Moscow/Urusi).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEMBA BA ATEMWA SENEGAL KIKOSI CHA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top