• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  AZAM FC YAPATA USHINDI WA KWANZA UGANDA

  AZAM FC imeshinda mechi yake ya kwanza jana katika ziara yake ya Uganda, baada ya kuwalaza wenyeji Vipers mabao 3-1 mjini Kampala. 
  Mabao ya Azam FC jana yalifungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche mawili na lingine Khamis Mcha ‘Vialli’.
  Awali, Azam FC inayofundishwa na makocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda, George ‘Best’ Nsimbe ilipoteza mechi mbili baada ya kufungwa 3-2 na SC Villa na 1-0 na URA.
  Kikosi cha Azam FC leo kinatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho katika ziara ya kambi ya wiki moja na zaidi, dhidi ya KCCA na kesho kitapanda ndege kurejea Dar es Salaam.
  Azam FC iliweka kambi huko kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo ilisimama tangu Novemba na itarejea wiki ijayo.
  Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, wanatarajiwa kuanza na Yanga SC katika raundi ya nane ya Ligi Kuu wiki ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mchezo ambao unatarajiwa kuwa ‘patashika nguo kuchanika’.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPATA USHINDI WA KWANZA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top