• HABARI MPYA

  Thursday, December 25, 2014

  GRANT AITA 33 KIKOSI CHA AWALI GHANA MATAIFA YA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, KUMASI
  KOCHA Myahudi wa Ghana, Avram Grant ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 31 kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea mwaka 2015.
  Grant amewastaajabisha wengi kwa kuwaita wachezaji ambao hawajawahi kuichezea Black Stars, Enoch Adu Kofi wa Malmo, Ibrahim Moro wa AIK Stockholm zote za Sweden, Daniel Amartey wa FC Copenhagen ya Denmark na Kwesi Appiah wa Cambridge United ya England.
  Kocha huyo wa zamani wa Chelsea ya England amemrejesha kikosini kipa Ernest Sowah wa Don Bosco ya DRC sawa na beki anayecheza Marekani, Samuel Inkoom na Alfred Duncan wa Sampdoria ya Italia.
  Avram Grant ameita wachezaji 33 kikosi cha awali Ghana

  Black Stars ambayo ilifika Nusu Fainali katika michuano yote mine iliyopita ya AFCON, imepangwa Kundi C na Algeria, Afrika Kusini na Senegal.
  Kikosi kamili ni makipa; Razak Braimah (Mirandes, Hispania), Adams Stephen (Aduana Stars), Fatau Dauda (AshGold) and Ernest Sowah (Don Bosco, DRC), mabeki; Harrison Afful (Esperance, Tunisia), John Boye (Erciyesspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Evian, Ufaransa), Jeffery Schlupp (Leicester City, England), Awal Mohammed (Maritzburg, Afrika Kusini), Kwabena Adusei (Mpumalanga Black Aces, Afrika Kusini), Baba Rahman (Augsburg, Ujerumani), Gyimah Edwin (Mpumalanga Black Aces, Afrika Kusini), Samuel Inkoom (Houston Dynamo, Marekani), Daniel Amartey, (FC Copenhagen, Denmark)
  Viungo; Rabiu Mohammed (Krasnodar, Urusi), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Parma, Italia), Solomon Asante (T.P. Mazembe, DRC), Christian Atsu (Everton, England), Mubarak Wakaso (Celtic, Scotland), Andre Ayew (Olympique Marseille, Ufaransa), Alfred Duncan (Sampdoria, Italia), Albert Adomah (Middlesbrough, England), Frank Acheampong (Anderlecht, Ubelgiji), Adu Kofi (Malmo, Sweden), Ibrahim Moro (AIK Stockholm, Sweden)
  Washambuliaji; Jordan Ayew (Lorient, Ufaransa), Abdul-Majeed Waris (Trabzonspor, Uturuki), Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Kwesi Appiah (Cambridge United, England), David Accam (Chicago Fire, Marekani).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRANT AITA 33 KIKOSI CHA AWALI GHANA MATAIFA YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top