• HABARI MPYA

  Tuesday, December 30, 2014

  KOCHA GUINEA AMBEBA MTUKUTU CONSTANT KIKOSI CHA AFCON

  Na Mwandishi Wetu, GUINEA
  KOCHA wa Guinea, Michel Dussuyer amemchukua Kevin Constant katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika licha ya kiungo huyo mtata kutokuwa na mahusiano mazuri na chama cha soka cha nchi hiyo.
  Mchezaji huyo wa Trabzonspor alilaumu uhusiano mbaya na wachezaji wenzake na vifaa duni katika timu ya taifa, kabla ya kuamua kujitoa kwenye timu hiyo Oktoba, ingawa baadaye alirejea.
  Hakucheza mechi za kufuzu, lakini Dussuyer amejenga imani na mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan, huku pia akiwarejesha wachezaji nane tu kutoka wale waliokwenda kwenye Fainali za 2012, mara ya mwisho Guinea ilipocheza michuano hiyo.
  Kevin Constant amechukuliwa kikosi cha mwisho Guinea Mataifa ya Afrika 

  Kikosi kamili cha Guinea kinaundwa na makipa; Abdul Aziz Keita (AS Kaloum), Naby Yattara (Arles Avignon) na Aboubacar Camara (Murcia), mabeki; Djibril Tamsir Paye (Zulte Waregem), Fode Camara (Horoya AC), Abdoulaye Cisse (Angers), Mohammed Diarra (Odense), Florentin Pogba (St Etienne), Baissama Sankoh (Guingamp), Issiaga Sylla (Toulouse) na Kamil Zayatte (Sheffield Wednesday).
  Viungo ni Kevin Constant (Trabzonspor), Ibrahima Conte (Anderlecht), Lanfia Camara (Mechelen), Boubacar Fofana (Nacional), Naby Keita (Red Bull Salzburg) na Bouna Sarr (Metz), wakati washambuliaji ni Abdoul Camara (Angers), Francois Kamano (Bastia) Seydouba Soumah (Slovan Bratislava), Idrissa Sylla (Zulte Waregem), Ibrahima Traore (Borussia Monchengladbach) na Mohamed Yattara (Lyon).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA GUINEA AMBEBA MTUKUTU CONSTANT KIKOSI CHA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top