• HABARI MPYA

  Thursday, December 25, 2014

  BRENDAN RODGERS ASEMA BALOTELLI HAENDANI NA MFUMO WA UCHEZAJI WA LIVERPOOL

  KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba mshambuliaji Mario Balotelli haendani na mfumo wa sasa wa uchezaji ya Wekundu hao wa Anfield.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao mawili tu tangu ajiunge na timu hiyo kutoka AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 16 Agosti mwaka huu na uamuzi wa sasa wa Rodgers unauweka shakani mustakabali wa Mtaliano huyo.
  Maisha yake ya Liverpool hayajatawaliwa na migogoro mingi hadi sasa, zaidi ya kufungiwa mechi moja na Chama cha Soka kwa kuposti mambo yaliyotafsiriwa kama udhalilishaji kwenye mitandao ya kijamii.  
  Mario Balotelli has failed to impress for Liverpool since joining from AC Milan in the summer
  Mario Balotelli ameshindwa kung'ara Liverpool tangu atue kutoka AC Milan 

  Kuelekea mechi na Burnley kesho, Rodgers amesema: "Nafikiri tumeona kwamba huo siyo mchezaji wake haswa (mfumo wa  3-4-3).
  "Nikiwa nimekwishafanya kazi na Mario aiwa hapa, tumeona kwamba mchezaji huyo ni mzuri anapocheza kwenye boksi, hivyo tunaoutumia kwa sasa hauwezi. Lakini unajaribu kufanya vizuei kutokana na wachezaji ulionao, na ubora ambao unao, hivyo hilo ndilo jambo tunalolifanyia kazi,"amesema.
  Brendan Rodgers has conceded that Balotelli doesn't suit Liverpool's current style of play
  Brendan Rodgers amesema Balotelli haiendani na mfumo wa uchezaji wa Liverpool
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRENDAN RODGERS ASEMA BALOTELLI HAENDANI NA MFUMO WA UCHEZAJI WA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top