• HABARI MPYA

  Monday, December 29, 2014

  MALI YATAJA KIKOSI CHA UBINGWA AFCON

  Na Mwandishi Wetu, BAMAKO
  KOCHA Msaidizi wa Mali, Cheick Omar Kone jana ametaja kikosi cha awali kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Equatorial Guinea, huku akimrejesha kikosini Modibo Maiga wa Metz baada ya muda mrefu.
  Abdou Traore na Cheick Diabate wote wa Bordeaux ya Ufaransa wamo kikosini, wakati kipa wa Ajaccio, Oumar Sissoko ametemwa.
  Kiungo wa zamani wa Barcelona, Seydou Keita, ambaye kwa sasa anachezea Roma ya Serie A, atakuwa Nahodha wa Tai hao kwenye mashindano hayo chini ya kocha Mpoland, Henry Kasperczak wakiwania kupiku rekodi ya fainali zilizopita Afrika Kusini, kushika nafasi ya tatu.
  Nahodha wa Mali, Saydou Keita
  Wachezaji wengine sita wamewekwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba.

  Mali wataweka kambini nchi jirani, Gabon kuanzia Januari 6 hadi 14 na watacheza mechi za kirafiki mbili na Afrika Kusini na Tunisia.
  Kikosi kamili cha Mali ni malipa; Soumaïla Diakite (Esteghlal Khuzestan, Iran), Germain Berthé (Onze Createurs), N’Tji Michel Samake (CS Duguwolofila, Mali).
  Mabeki; Drissa Diakite (Bastia, Ufaransa), Fousseyni Diawara (Tours, Ufaransa), Molla Wague (Udinese, Italia), Ousmane Coulibaly (Platanias, Ugiriki), Adama Tamboura (Randers, Denmark), Idrissa Coulibaly (Hassania Agadir, Morocco), Salif Coulibaly (TP Mazembe, DRC, Mohamed Konaté (Renaissance Berkane, Morocco).
  Viungo: Seydou Keïta (AS Rome, Italia), Tongo Hamed Doumbia (Toulouse, Ufaransa), Yacouba Sylla (Erciyesspor, Uturuki), Mamoutou N’Diaye (Zulte Waregem, Ubelgiji), Abdou Traoré (Bordeaux, Ufaransa), Ibourahima Sidibé (MAS Fès, Morocco), Souleymane Diarra (AS Réal), Idrissa Traoré (Stade Malien), Sigamary Diarra (Valenciennes, Ufaransa).
  Washambuliaji; Cheick Tidiane Diabaté (Bordeaux, Ufaransa), Bakary Sako (Wolverhampton, Angleterre), Mustapha Yatabaré (Trabzonspor, Turquie), Sambou Yatabaré (Guingamp, Ufaransa), Abdoulaye Diaby (Mouscron, Ubelgiji) na Modibo Maïga (Metz, Ufaransa), wakati Abdoulay Samake (CO Bamako), Khalifa Traoré (SCO Angers), Idrissa Traoré (Stade Malien), Souleymane Diarra (AS Réal), Mohammed Traoré (El Merreikh) na Cheick Fantamady Diarra (Auxerre) wamewekwa katika orodha ya wachezaji wa akiba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALI YATAJA KIKOSI CHA UBINGWA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top