• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  DROGBA ATEMWA KIKOSI CHA IVORY COAST MATAIFA YA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, ABIDJAN
  KOCHA wa Ivory Coast, Herve Renard ametaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachosafiri kwenda kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika Equatorial Guinea bila mkongwe Didier Drogba (pichani kushoto).
  Timu hiyo itaweka kambi Abu Dhabi kuanzia Januari 5 hadi 16, mwaka 2015 kabla ya michuano hiyo ambayo watacheza mechi zao Malabo.
  Renard hajawaita wakongwe Drogba na Didier Zokora ambao walistaafu soka ya kimataifa kutokana na umri. 
  Tembo wa Ivory Coast watachea mashindano hayo kwa mara ya 21, wakiwa kutwaa taji la pili tangu walipotwaa la kwanza mwaka 1992.
  Kikosi kamili ni makipa; Gbohouo Sylvain (Sewe),
  Mande sayouba (Staebek) na Coppa Barry (Lokeren), mabeki; Aurier Serge (PSG), Tiene Sakia (Montpelier), Viera Ousmane (Rizesport), Kolo Toure ( Liverpool ), Wilfried Kanon (ADO), Eric Bertrand Bailly (RCD Espanyol) na Akpa Akpro Jean-Daniel (Toulouse).
  Viungo ni; Diomande Ismael (St Etienne), Yaya Toure (Manchester City), Serey Die Geoffrey (Bale), Doukouré Cheick (Metz), Tiote Cheick (Newcastle), Gradel Max (St Etienne) na Assale Roger (Sewe San Pedr) na washambuliaji Gervinho (AS Roma), Kalou Salomon (Hertha Berlin), Traore Lacina (Monaco), Tallo Junior (Bastia), Bony Wilfried (Swansea) na Seydou Doumbia (CSKA Moscow).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DROGBA ATEMWA KIKOSI CHA IVORY COAST MATAIFA YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top