KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Mossi Nduwumwe ameibuka Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kumaliza msimu na mabao 16, moja zaidi ya mzawa, Feisal Salum Abdallah wa Azam FC.
Mossi ametokea nyuma kumpiku Feisal aliyekuwa anaongoza baada ya kufunga matatu dakika ya tisa, 12 na 86, ingawa timu yake, Singida Black Stars imefungwa 4-3 na wenyeji, Fountain Gate FC jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Kwenye mchezo huo, mabao ya Fountain Gate FC yamefungwa na Wanigeria, kiungo Henry David dakika ya tano, mshambuliaji Obasi MacDonald Chukwunonye dakika ya 26 na mshambuliaji chipukizi, Hashimu Omary Kindemile aliyefunga mawili dakika ya 66 na 67.
Mganda Allan Jolly Okello ‘Star Boy’ wa Yanga SC amemaliza na mabao 14 mbele ya washambuliaji Fabrice Ngoy wa Namungo FC, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mkenya Mathew Tegisi Momanyi wa Pamba Jiji ambao kila mmoja amefunga mabao 11.
Mossi anaingia kwenye orodha ya wachezaji wa Burundi waliowahi kuwa Wafungaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanznaia Bara – akiwemo Didier Kavumbagu msimu wa 2013–2014 alipofungana na mchezaji mwenzake wa Yanga, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma ka kila mmoja kufunga mabao 16.
Wengine ni Amissi Joselyn Tambwe msimu wa 2015–2016 aliyefunga mabao 21 akiwa Yanga SC na Saido Ntibazonkiza akiwa Simba SC msimu wa 2022–2023 alipofungaa na Mkongo Fiston Kalala Mayele w aYanga kwa kila mmoja kufunga mabao 18.



.png)
0 comments:
Post a Comment