• HABARI MPYA

  Tuesday, December 30, 2014

  MAREFA 18 WAPATA BEJI ZA FIFA

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  WAAMUZI 18 wa Tanzania wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2015.
  Idadi hiyo ambayo ni rekodi kwa Tanzania inahusisha waamuzi saba wa kike. Waamuzi wa kati wa kike waliopata beji hizo ni pamoja na Jonesia Rukyaa Kabakama aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga. Wengine ni Florentina Zablon Chief na Sophia Ismail Mtongori.
  Waamuzi wasaidizi wa kike waliopata beji hizo ni Dalila Jafari Mtwana, Grace Wamala, Hellen Joseph Mduma na Kudura Omary Maurice.
  Israel Nkongo kulia naye amepata beji mpya ya FIFA

  Kwa waamuzi wa kati wa kiume ni Israel Mujuni Nkongo, Martin Eliphas Sanya, Mfaume Ali Nassoro na Waziri Sheha Waziri. Waamuzi wasaidizi ni Alli Kinduli, Ferdinand Chacha, Frank John Komba, John Longino Kanyenye, Josephat Deu Bulali, Samuel Hudsin Mpenzu na Soud Iddi Lila.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAREFA 18 WAPATA BEJI ZA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top