• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  MAN CITY YAIKAMATA CHELSEA KILELENI ENGLAND

  MABINGWA watetezi, Manchester City wamefikia Chelsea kwa pointi kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 jioni ya leo dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Etihad.
  Huku Sergio Aguero, Edin Dzeko na Stevan Jovetic wakiwa majeruhi, James Milner alianza katika nafasi ya kiungo na David Silva akafunga bao la kwanza akicheza mechi ya 200 kwa The Blues dakika ya 49. 
  ‘Mchawi huyo’ akaifungia City bao la pili akimalizia krosi ya Alexsander Kolarov dakika ya 61, kabla ya Yaya Toure kufunga la tatu dakika ya 79 akimalizia pasi ya Milner.
  City imeshinda mechi nane mfululizo Ligi Kuu England, lakini bao la nne lingewapika kileleni kwa wastani mzuri wa mabaio.
  Manchester City; Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Kolarov, Toure, Fernandinho, Navas, Silva/Lampard dk68, Nasri/Sinclair dk88 na Milner/Fernando dk80.
  Crystal Palace; Speroni, Kelly, Hangeland, Dann, Ward, Jedinak, McArthur, Ledley/Bannan dk88, Puncheon/Thomas dk83, Campbell/Zaha dk65 na Bolasie.
  David Silva (right) struck his second goal after the interval to send the champions right back into the title race
  David Silva (kulia) akifunga bao la pili
  Yaya Toure completed the rout with his side's third goal from a thunderous strike towards the end of the game
  Yaya Toure akifunga bao la tatu

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2881683/Manchester-City-3-0-Crystal-Palace-David-Silva-Yaya-Toure-fire-striker-light-champions-level-Chelsea-table.html#ixzz3MS2YNWMm 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIKAMATA CHELSEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top