• HABARI MPYA

  Monday, December 29, 2014

  KAVUMBANGU ATIMIZA MABA0 10 AZAM FC

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu jana amefunga bao lake la 10 katika klabu ya Azam FC, ikitoa sare ya 2-2 na timu yake ya zamani, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kavumbangu aliifungia Azam FC bao la kwanza dakika ya tano, kabla ya Mrundi mwenzake, Amisi Tambwe kuisawazishia Yanga SC dakika ya saba.
  Simon Msuva akaifungia Yanga SC bao lililoelekea kuwa la ushindi mapema kipindi cha pili, kabla ya John Raphael Bocco aliyetokea benchi kwenda kuisawazishia Azam FC.
  Didier Kavumbangu amefunga bao lake la 10 jana Azam FC
  Didier Kavumbangu akiwatoka wachezaji wa timu yake ya zamani jana, Yanga SC

  Kavumbangu amefunga mabao 10 katika mechi 18 za mashindano yote tangu asajiliwe Azam FC Julai mwaka huu kutoka kwa wapinzani, Yanga SC na matano kati ya mabao hayo, amefunga katika Ligi Kuu.
  Awali, katika misimu yake miwili ya kuichezea Yanga SC akitokea Atletico ya Burundi, Kavumbangu alifunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote. Kufikisha mabao 10 katika mechi 18, maana yake Kavumbangu anaweza kufanya vizuri zaidi Azam FC, endapo ataendeleza moto huo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU ATIMIZA MABA0 10 AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top