• HABARI MPYA

  Monday, December 29, 2014

  ZABALETA ALIVYOONYESHA UJASIRI WAKE JANA MAN CITY

  BEKI wa Manchester City, Pablo Zabaleta jana alionyesha moyo wa ujasiri baada ya kucheza akivuja damu kufuatia kuchanika sehemu ya juu ya jicho lake la kushoto katika mchezo ambao timu yake ilitoa sare ya 2-2 na Burnley Uwanja wa Etihad.
  Beki huyo wa pembeni aligongana na mchezaji mwenzake, Eliaquim Mangala wakati wanawania mpira na kuchanika sehemu ya kichwani kiasi cha kutokwa damu nyingi kipindi cha kwanza.
  Picha zinamuonyesha mchezaji huyo wa Argentina akipatiwa huduma ya kwanza na timu ya madaktari wa City baada ya kuumia juu ya jicho lake la kushoto.
  The 29-year-old was laid stricken on the floor as the City medical team attended his bloody injury
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia jana
  Zabaleta's on-field treatment included an injection into his forehead from the Manchester City medical team
  Zabaleta alitibiwa na akarejea uwanjani kumalizia mchezo
  Zabaleta (centre) lays still as the City medical staff patch him up with a bandage around his head
  Zabaleta (katikati) akifungwa bandeji na madaktari wa City jana

  Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 alirejea uwanjani kumalizia mchezo baada ya kufungwa bandeji kichwani.
  Katika mchezo huo, David Silva na Fernandinho walitangulia kuifungia City kabla ya George Boyd na Ashley Barnes kusawazisha.

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2889307/Pablo-Zabaleta-suffers-gruesome-head-injury-leaves-head-split-open-Manchester-City-draw-home-Burnley.html#ixzz3NHJU9o1z 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZABALETA ALIVYOONYESHA UJASIRI WAKE JANA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top