• HABARI MPYA

  Sunday, December 28, 2014

  JOHN TERRY APEWA MKATABA MPYA CHELSEA

  BEKI John Terry atasaini Mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Chelsea baada ya kocha Mreno, Jose Mourinho kusema mpango huo unaandaliwa.
  Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 34 ataongoza mbio za kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwa wa Kulipwa (PFA) kutokana na kufanya kwake vizuri hivi sasa akicheza katika safu ya ulinzi. 
  Chelsea have acted quickly to reassure John Terry that he will remain at Stamford Bridge
  Chelsea imemuhakikishia mkongwe John Terry kuendelea na kazi Stamford Bridge

  Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesema jana kwamba Terry bado mchezaji muhimu kwake. "Hakuna shaka atapewa Mkataba mwingine. Nafahamu hilo, anafahamu pia. Tupo katika klabu, katika bodi tunafahamu hilo na pia unatakiwa kufikiria hilo,".
  "Bila sisi kuthibitisha hilo, unatakiwa ufikirie hivyo. Ni mchezaji muhimu sana katika timu, hivyo mkataba mpya unakuja haraka iwezekanavyo. Ni utaratibu tu," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOHN TERRY APEWA MKATABA MPYA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top