• HABARI MPYA

  Sunday, December 21, 2014

  REAL MADRID WATWAA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA KWANZA

  MABAO ya Sergio Ramos na Gareth Bale yameipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya San Lorenzo na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia jana Uwanja wa Marraksh, Morocco.
  Beki wa kimataifa wa Hispania, Ramos alifunga bao la kwanza dakika ya 37 kabla ya Bale kufunga la pili dakika ya 51.
  Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Real Madrid kutwaa taji hilo la dunia, baada ya kuifunga timu ngumu Amerika Kusini, ambao ni mabingwa wa bara lao.
  Aidha, Real inafikisha mechi ya 22 kushinda kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal/Arbeloa dk73, Pepe, Sergio Ramos/Varane dk89, Marcelo/Fabio Coentrao dk44, Ronaldo, Kroos, Rodriguez, Bale, Isco na Benzema.
  San Lorenzo: Torrico, Yepes/Cetto dk61, Mas, Kannemann, Mercier, Buffarini, Kalinski, Barrientos, Ortigoza, Cauteruccio Rodriguez/Matos dk68 na Veron/Romagnolidk 57.
  Real Madrid captain Iker Casillas (centre) lifts the FIFA Club World Cup trophy after they beat San Lorenzo 2-0
  Nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas (katikati) akiinua Kombe la Dunia la FIFA jana baada ya kuifunga San Lorenzo 2-0

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2882085/Real-Madrid-2-0-San-Lorenzo-Sergio-Ramos-Gareth-Bale-score-European-champions-win-Club-World-Cup.html#ixzz3MVWJUhmi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID WATWAA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top