• HABARI MPYA

  Wednesday, December 24, 2014

  LIGI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA KRISMASI

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  LIGI Daraja la Pili (SDL) inayochezwa katika makundi manne tofauti inaingia raundi ya nne kesho (Desemba 25 mwaka huu) kwa mechi ya kundi C kati ya Kiluvya United na Abajalo itakayochezwa Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
  Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Mshikamano FC na Transit Camp yenyewe itachezwa keshokutwa (Desemba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
  Kundi A litakuwa na mechi Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) ambayo itazikutanisha timu za Ujenzi Rukwa na Mji Mkuu (CDA) kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Desemba 28 mwaka huu ni kati ya Mvuvumwa FC na Milambo SC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) kundi B litakuwa na mechi kati ya Arusha FC na Pamba (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha), na Mbao FC vs JKT Rwamkoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
  Kikosi cha CDA kitacheza na Ujenzi Rukwa

  Kundi D siku ya Jumamosi hekaheka itakuwa kati ya Mkamba Rangers na Volcano (Uwanja CCM Mkamba), Njombe Mji vs Wenda FC (Uwanja wa Amani, Njombe) na Town Small Boys vs Magereza FC (Uwanja wa Majimaji, Songea).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA KRISMASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top