• HABARI MPYA

  Sunday, December 28, 2014

  MTIBWA SUGAR NA STAND UNITED SARE 1-1 MANUNGU

  Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime
  MTIBWA Sugar imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Stand United katika mwendelezo wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara asubuhi ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  Mchezo huo ulivunjika dakika ya sita jana kutokana na mvua na ukaendelea asubuhi ya leo na timu hizo kufungana 1-1. 
  Mtibwa inabaki kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 16 baada ya mechi nane, ikifuatiwa na Azam FC na Yanga zenye pointi 13 kila mmoja baada ya mechi saba, ambazo zinamenyana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA STAND UNITED SARE 1-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top