• HABARI MPYA

  Sunday, December 28, 2014

  CHELSEA YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU ENGLAND

  CHELSEA imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa St Mary’s. 
  Sadio Mane alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 17 akimvisha kanzu kipa Thibaut Courtois, kabla ya kiungo Eden Hazard kuisawazishia Chelsea kabla ya mapumziko.
  Southampton ilimaliza mechi hiyo pungufu ya mchezaji mmoja, baada ya Morgan Schneiderlin kutolewa kwa kadi ya pili ya njano.
  Kikosi cha Southampton kilikuwa; Forster, Yoshida/Gardos dk62, Fonte, Alderweireld, Targett, Schneiderlin, Wanyama, Davis/Long dk77, Mane, Tadic/Ward-Prowse dk58 na Pelle.
  Chelsea; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Obi/Drogba dk74, Matic, Schurrle, Fabregas, Hazard na Costa/Remy dk89.
  Cesc Fabregas goes down in the penalty area after a challenge by Southampton youngster Matt Targett
  Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas akienda chini kwenye eneo la penalti baada ya kukumbana na kinda wa Southampton, Matt Targett

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2889160/Southampton-1-1-Chelsea-Eden-Hazard-cancels-Sadio-Mane-s-opener.html#ixzz3NDF5IylW 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top