• HABARI MPYA

  Wednesday, December 31, 2014

  WENGER ANAKABILIWA NA TATIZO LA WASHAMBULIAJI KUELEKEA MECHI NA SOUTHAMPTON KESHO

  KOCHA Arsene Wenger anakabiliwa na tatizo la washambuliaji kuelekea mechi dhidi ya Southampton kesho, kufuatia Danny Welbeck kupata maujibu ya nyama za paja.
  Huku Olivier Giroud akiwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, Welbeck alitarajiwa kucheza kama mshambuliaji pekee katika siku ya kwanza ya mwaka mpya.
  Lakini mshambuliaji huyo wa England yuko shakani sasa kwenda Uwanja wa St Mary’s, maana yake Wenger atakuwa bila mshambuliaji halisi kesho.
  Danny Welbeck is doubtful for Arsenal's trip to Southampton after picking up a thigh injury 
  Danny Welbeck yuko shakani kusafiri na Arsenal kuwafuata Southampton baada ya kuumia nyama za paja
  Olivier Giroud is also suspended for the Gunners leaving Arsenal with a striking crisis ahead of trip
  Olivier Giroud anatumikia adhabu ya kadi nyekundu

  Wenger amethibitisha: "Tuna shaka ya mtu mmoja kwa sasa baada ya mechi na West Ham na huyo ni Danny Welbeck, anaweza kukosekana Alhamisi,".
  Lukas Podolski anatarajiwa kupewa jukumu la kucheza katika nafasi ya ushambuliaji iwapo Welbeck hatapata ahueni, na Theo Walcott ndiyo kwanza anarejea kutoka kwenye majeruhi. 
  Wenger pia amesema kwamba Aaron Ramsey hatakuwa fiti kwa safari 'akiwawakia' Inter Milan kwa ofa yao kutaka kumsajili Podolski.
  Klabu hiyo ya Serie A inataka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji huyo wa Ujerumani hadi mwishoni mwa msimu, mara tu dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER ANAKABILIWA NA TATIZO LA WASHAMBULIAJI KUELEKEA MECHI NA SOUTHAMPTON KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top