• HABARI MPYA

  Monday, December 22, 2014

  KOCHA WA TIMU YA TAIFA UGANDA ATUA STAND UNITED

  Na Philipo Chimi, SHINYANGA
  TIMU ya Stand United ya Shinyanga ‘Chama la Wana’, imemuajiri kocha Mganda, Mathia Lule kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Lule aliyewahi kuzinoa timu za KCCA, Express na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya nchi hiyo, The Kobs amesaini Mkataba wa miezi sita leo kupiga kazi ‘Shy Town’.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini hapa, Mkurugenzi wa bench la ufundi la timu hiyo, Muhibu Kanu amesema kwamba wamemchukua kocha huyo ili kuimarisha benchi lao la ufundi.
  Kocha mpya wa Stand United, Mathia Lule ameahidi furaha kwa mashabiki

  Amesema kocha huyo mpya atasaidiwa na waliokuwa makocha wa timu hiyo tangu inapanda daraja, Emmanuel Massawe na Athumani Bilal.
  Kwa upande wake, Lule amesema amefurahishwa kutua Stand Utd na ameipongeza timu hiyo kwamba ina wachezaji wazuri na wenye vipaji vya hali ya juu, hivyo kuwaahidi furaha mashabiki.
  “Stand ni timu nzuri, wachezaji wake wana vipaji, hivyo nawaomba mashabiki watuunge mkono, naamini tutafanya vizuri mara baada ya ligi kuanza,”amesema Lule.
  Tayari Stand United imeimarisha kikosi chake katika dirisha dogo la usajili kwa kuongeza nyota kama winga Haruna Chanongo kutoka Simba kwa mkopo, Hamisi Thabiti kutoka Yanga, Jamir Mchaulu ‘Balotelli’ kutoka Azam Academy, Chinn Eddy kutoka Enyimba ya Nigeria na Shaaban Kondo kutoka Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA TIMU YA TAIFA UGANDA ATUA STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top