• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  FALCAO AINUSURU MAN UNITED KULALA VILLA PARK

  BAO la Radamel Falcao dakika ya 52 limeunusuru Manchester United kulala mbele ya Aston Villa baada ya kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Villa Park jioni ya leo.
  Villa ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya mchezaji wake, Gabriel Agbonlahor kutolewa kwa kadi nyekundu katikati ya kipindi cha pili baada ya kumchezea rafu Ashley Young.
  Lakini iliweza kupata bao la kuongoza dakika ya 18 kupitia kwa Christian Benteke aliyefumua shuti kwa mguu wa kushoto, kabla ya Falcao kuunganishwa kwa kichwa krosi ya Ashley Young kuisawazishia United.
  Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Guzan, Okore, Vlaar, Clark, Lowton, Sanchez, Delph, Weimann/N'Zogbia dk80, Cissokho/Bacuna dk80, Benteke na Agbonlahor
  Man Utd; De Gea, Jones, Carrick, Evans, Valencia/Wilson dk74, Fletcher/Fletcher dk46, Rooney, Mata, Young, Van Persie/Di Maria dk62 na Falcao. 
  Radamel Falcao (second left) scored United's equaliser heading home from an Ashley Young cross on 53 minutes
  Radamel Falcao (wa pili kushoto) akiwa hewani kupiga kuifungia United bao la kusawazisha kwa krosi ya Ashley Young dakika ya 53
  The on loan Monaco striker is hugged by his Red Devils team-mates after putting them on level terms with Villa
  Mchezaji wa mkopo kutoka Monaco akipongezwa na wenzake baada ya kjuwasawazishia Mashetani Wekundu dhidi ya Villa

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2881816/Aston-Villa-1-1-Manchester-United-Radamel-Falcao-cancels-Christian-Benteke-s-strike-visitors-winning-league-streak-ends.html#ixzz3MSi6mLpe 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FALCAO AINUSURU MAN UNITED KULALA VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top